Tuesday, January 31, 2012

........POLE RIYAMA MUNGU ATAKUSAIDIA......


RIYAMA yupo hoi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya jino yaliyomuanza alipokuwa kwenye kazi zake za kurekodi filamu.
Awali hakuhisi kama jino hilo lingeweza kumletea maumivu kama ilivyotokea.

"Kuumwa kusikie tu kwa mtu tena hasa ugonjwa kama wa jino, lina maumivu makali sana kumbe mtu unaweza kuondoka Dunia kwa muda mfupi tu na watu wakashangaa kuwa mbona alikuwa haumwi? Kumbe jino limemletea maumivu makubwa na kushindwa kuvumilia,"anasema Riyama.

Kwa sasa msanii huyo anaendelea vizuri baada ya uvimbe uliotokana na maumivu hayo ambao ulibadilisha hata mwonekano wa sura yake kupungua.

Riyama ni moja kati ya wasanii wakongwe wanaotamba katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu, filamu alizoshiriki na kuvuma sana ni pamoja na Fungu la Kukosa, My Darling, Alfa na Omega.

1 comments:

priss said...

ndo umejichubua au photopoint??

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms