Friday, January 27, 2012

...... MYAMBA AFUNGUA CHUO CHA FILAMU...........

MWIGIZAJI Mahiri katioka tasnia ya filamu Bongo Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amefungua chuo kwa ajili ya wasanii wachanga na wakongwe wapate fursa ya kujiongezea ujuzi kitaaluma ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la filamu kimataifa akiongea, Myamba amesema kuwa kutokana na uzoefu ambao amekuwa katika tasnia hiyo kwa Bongo amejifunza mengi na kugundua moja kati ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya tasnia hiyo ni pamoja na suala la Elimu.
“Nimekuwa katika tasnia ya filamu kwa muda sasa lakini kuna changamoto nyingi katika tasnia ya filamu, na jambo ambalo nimeliona ni wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii maskini wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo, lakini pia kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa shida kwao, na mwito ni mkubwa kweli,”anasema Pastor Myamba.
Chuo hicho kinachojulikana kwa jina Tanzania Film Training Center (TFTC) kipo maeneo ya Ubungo na tayari kina wanafunzi zaidi ya mia, Myamba amesisitiza wasanii wengine kujitokeza katika chuo ili waweza kujijenga zaidi katika masuala ya uigizaji na kujenga sanaa bora ili kuelekea katika soko la kimataifa huku akiongelea ushindani kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, itakapoanza inaweza kutupoteza watanzania kwa kukosa elimu kuhusu fani tunazofanya.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms