Saturday, January 21, 2012

.........MESEJI HII NI MUHIMU SANA KWAKO MDAU WA WAJANJA BLOG..........PLEASE READ IT.............

 Huu ndo mlango wa kuingia Ambaoni Caves



WAJANJA BLOG TEAM (WBT), binafsi nawashukuru sana kwa kuendelea kutuletea habari motomoto kwani mmekuwa chanzo kizuri cha habari hapa nchini. Pamoja na hayo mazuri mnayoyafanya mpaka blog hii ikawa blog pendwa kwa watanzania wote hasa vijana, nami leo naomba mnifikishie meseji hii kwa watanzania wenzangu wote but tafadhari msiweke picha yangu cz jamaa ana wivu sana, hahahaha.

Last week, my best friend aliniomba nimsindikize Tanga kwa ajili ya mapumziko yake mafupi, bila hiana nilikubali na kuandamana naye. Safari ilikuwa ndefu sana kwani njia nzima mie nilikuwa mtu wa kusinzia tu, safari yetu ilianza saa tatu asubuhi na tulifika saa kumi jioni.

Kwa vile tulikuwa tumechoka wote, siku hiyo tuliitumia kulala tu. Kesho yake rafiki yangu aliniomba tuende AMBONI CAVES ili kuisindikiza weekend yetu.
Lol sikuamini niliyoayaona huko AMBONI CAVES, kwa siku hiyoo tuliweza kutembelea caves mbili tu, ile kubwa na ile ndogo inayoenda kwa jina la GENDER CAVE.

Kwa ujumla watanzania tumebarikiwa jamani kwani AMBONI CAVES kuna maajabu ambayo yanadhihilisha kabisa kuwa mungu yupo. Inasemekana kuwa AMBONI CAVES miaka kadhaa huko nyumba ilikuwa ardhini na ilitengenezwa na maji. Ni pazuri sana kwani maji yaliweza kutengeneza vitu vingi sana kama vile; kanisa, msikiti, biblia, wanyama, ramani ya Africa, mguu wa tembo, kichwa cha tembo, mlima Kilimanjaro na vitu vingine vingi.

Na kwa upende wa GENDER CAVES, maji yaliweza kutengeneza sehemu za siri za binadamu. Weekend hiyo ilikuwa ya maajabu kwangu kwani kwani ndo ilikuwa mara ya kwanza kufika AMBONI CAVSE, yaani HAKUNAGA TENA. Tulitumia masaa kama mawili tukivinjari ndani ya mapango hayo.
Kama hujawahi kwenda AMBONI CAVES nakuomba uende ukashudie maajabu ya mungu.

Ni mimi,
Dada Eva.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms