Wednesday, January 25, 2012

........MATATIZO YAZIDI KUMZONGA BABY MADAHA........


MATATIZO yanaendelea kumkabili msanii wa filamu bongo, Baby Madaha, baada ya sasa kufikishwa kituo cha polisi cha Oysterbay kwa madai ya utapeli wa shilingi laki 500,000, kutoka kwa kampuni moja inayohusika na masuala ya urembo ambapo jana ametolewa kwa dhamana na familia yake.

Awali nyota huyo alidaiwa kuwatapeli wasanii chipukizi kiasi cha shilingi laki 300,000, ingawa hawakuweza kumfikisha popote.

Chanzo cha habari cha kuaminika kilichozungumza na mtandao huu, kilisema kuwa msanii huyo alikopa kiasi hicho cha fedha kwa madai kuwa rafiki yake wa karibu anaumwa hivyo alihitaji kiasi hicho ili ziweze kumsaidia katika matibabu.

Kilisema kuwa baada ya kukopa fedha hizo aliamua kutoroka jijini na kwenda kuishi Morogoro, kitu ambacho kiliwapa mashaka watu ambao walimkopesha fedha hizo na kwenda kutoka taarifa kituo cha polisi.

“Siwezi kusema kama ni kweli alikuwa na nia ya kutapeli lakini kwanini baada ya kupewa fedha hizo aliamua kwenda kuishi Morogoro, wakati makazi yake yapo hapa jijini tena baada ya kupewa fedha hizo tu,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Baada kupata ishu hiyoBaby Madaha alitafutwa ili kujua undani wa habari hiyo lakini baada ya kupatikana alionekana  kujibu kwa wasiwasi kama mtu ambaye amekamatwa na dawa za kulevya

Baada ya maswali kadhaa aliamua kufunguka na kusema kuwa hajatapeli fedha hizo na alienda Morogoro kwa matatizo yake, lakini habari za kufikishwa polisi hazina ukweli kwani alienda kituo cha polisi kwa ajili ya mazungumzo rafiki na mmoja wa askari wa kituo hicho.

Alisema kuwa ni kweli amekopa kiasi hicho cha fedha lakini amezifanyia kazi ambayo ilimfanya akope na si vinginevyo.

Aliongeza kuwa kuna wimbi la wasanii limepanga kumchafulia jina lakini hana wasiwasi kwani hakuna anayempa kula.

“Hizo habari hazina ukweli kwani sina tabia ya kutapeli ingawa fedha hizo nilichukua, pia nilienda pale polisi  kwa kazi zangu si kwamba niliwekwa ndani,” alisema.

1 comments:

priss said...

he shost umefulia kiasi hucho laki tatu inakushina mpaka unakopa

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms