Monday, January 16, 2012

........MAKUNDI YATAUA SANAA NCHINI.......


MSANII wa filamu nchini, SHILOLE pichani juu, ambeye kusema kweli mimi binafsi nakubali sana kazi zake amefunguka na kusema kuwa makundi yanayoendelea ndani ya kiwanda cha filamu nchini yataua sanaa. Mrembo huyu amesema kuwa mwaka huu wa 2012 uwe mwaka wa wasanii hasa wa kike kupendana na kuachana na makundi yasiyokuwa na tija katika jamii na katika sanaa kwa ujumla. 
Hali kadhalika mwanadada huyu aliongeza kwa kusema kuwa msanii unatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na mashabiki wako na si kuwa kichefuchefu mbele ya mashabiki wako, aliongeza kwa kusema kuwa wasanii tunatakiwa kuachana na makundi yasiyokuwa na tija kwenye sanaa. Tupendane na tuungane ili tusonge mbele kwa pamoja...

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms