Thursday, January 5, 2012

.......KANUMBA NA RAY HAYA MLIYOYAAHIDI MTAYATIMIZA MWAKA 2012????.......


MWAKA 2012 utakuwa wa shangwe kwetu, haya ni maneno kutoka kwa wasanii Kanumba na Ray, hata hivyo wameka wazi kuwa baada ya mwaka uliopita kushindwa kutimiza malengo yao ya kuvuta jiko sasa wanajipaga mwaka huu ili waweze kuepukana na upweke na dowea dowea.
nyota hao wenye mafanikio makubwa katika tasnia hiyo, walisema kuwa umri wao unazidi kwenda hivyo hawanabudi kuchukua mke ili waanze kujenga familia.
Kwa upande wake Kanumba, alisema kama mwaka jana hakufanya hivyo basi mwaka huu lazima atimize ndoto yake ambayo hata ndugu na jamaa zake watafurahi kuhusu hilo ingawa anaomba mungu ampatia mke mwema anayejali familia na siyo yule ambaye anapenda kujirusha.
Alisema kuwa anaamini hata hivyo mungu yupo na yeye kwani, hataki kupata mke ambaye atampenda kwa kuwa yeye ni msanii ambaye atakuwa na malengo yake binafsi na siyo kuleta maendeleo katika kulea watoto watakazaa pamoja.
“Napenda kuwa na mke mcha mungu kwa sababu nimeshuhudia ndoa nyingi za watu zikiyumba kwa sababu hakuna upendo wa mungu ndani yake hivyo kwa upande wangu naonekana kimya katika hili siyo kwamba napenda kuwa hivi hapa najalibu kuchunguza tabia za kila mtu ambaye naweza kufunga naye ndoa,” alisema.
Naye Ray alisema anapenda kuishi na mke ambaye hana makuu kwa sababu anaamini endapo atapata mwanamke ambaye anapenda starehe basi hata watakachovuna kwani pesa zote zinaweza kuishia huko huku watoto.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms