Tuesday, January 31, 2012

.......HUU NI USHIRIKIANO MZURI - MJATTA.......

MTAYARISHAJI na Mwigizaji wa filamu Bongo, Eliya Mjatta David Bwana Mayenje yupo katika maandalizi ya mchezo wa hisani ambao utawakutanisha wasanii wa Komedi na wasanii wengine.

Mchezo huo utachezwa jumapili ijayo na amesema ni maalumu kwa ajili kuchangia wahanga wa mafuriko yaliyotokea na kupoteza makazi ya waathirika wa mafuriko jijini Dar es Salaam, mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Taifa siku hiyo ya tarehe Februari 5, 2012.

Tumeguswa sana na tukioa hilo la maafa yaliyotoke kwa wenzetu ambao wengine walipoteza maisha mali na makazi pia, sisi kama wasanii tumeamua kuwachangia kwa kucheza na wanamuziki wa Dansi na kiingilio ni 2000 tu kila mpenzi wa wasanii hasa wachekeshaji afike tuwachangie wenzetu, anasema Bwana Mayenje.

Gwiji la Vichekesho Bongo King Majuto ameahidi kufunga goli mbili pekee yake kwa mguu wake, huku kipa wa wanamuziki wa Dansi Nyoshi El Sadat akiapa kutoruhusu gori hata moja mchezo huu umeandaliwa na kampuni ya Campact Media ya jijini Dar es Salaam Jumapili ijayo

1 comments:

priss said...

manajitahidi

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms