Friday, January 27, 2012

.........BAADA YA KUTANGAZA KUACHANA NA KUIGIZA, SASA HEMEDI AFYATUA FILAMU MBILI KWA MPIGO........

NYOTA ndani ya bongo movie Hemed Suleiman ‘Hemed’,alizungumza na kusema ndani ya mwezi Februari anatarajia kutoa filamu zake mbili ambazo ni ‘Red Cross’ na ‘Shortcut’, ambazo ndizo zitakazo mtambulisha kwa mwaka huu wa 2012.

Hemedi alisema kuwa katika filamu ambayo imempa wakati mgumu tangu alipoanza kufanya kazi hiyo ni ‘Red Cross’, ambayo ilikuwa na matukio mengi likiwemo la kuisaliti dini yake ya Kiislamu.

Alisema baadhi ya matukio hayo ni pamoja na kuigiza kama mkristo wakati yeye ni Muislamu pamoja na kutamka maneno ya Kikristo kutoka ndani ya Biblia.

Aliongeza sambamba na matukio hayo pia alitumia nguvu nyingi kwani baadhi ya vipande vya kazi hiyo vinamuonyesha akikimbizwa na pikipiki sehemu ambazo zilikua na mabonde makubwa.

“Kazi ya Red Cross, naweza kusema ni filamu ambayo itakuwa tishio kwani matukio ambayo yanaonekana katika picha hiyo ni zaidi ya movie ambazo zimewahi kutoka hapa nchini,” alisema.

Sambamba na ujio wa filamu hizo pia aliongeza  kwa upande wa muziki anatarajia kutoa albamu yake aliyoipa jina la ‘Hedent’ ambayo itakuwa na nyimbo 13.

“Kwa upande wa muziki natarajia kutoa albamu hiyo, ambapo naamini itauza kwa sababu ina nyimbo ambazo zinaubora wa kimataifa,” aliongeza.

1 comments:

priss said...

tunasubiri tuone

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms